In Summary
  • Moto ambao chanzo chake hakikuweza kufahamika, leo mchana Ijumaa Novemba 9, 2018 umeteketeza moja ya jengo la Hoteli ya Bwawani iliyopo wilayani Handeni jijini Tanga

Handeni. Moja ya jengo la hoteli maarufu wilayani Handeni jijini Tanga ya Bwawani Cottages limeteketea kwa moto huku kukiwa hakujaokolewa kitu.

Moto huo ambao chanzo chake hakikuweza kufahamika, umeanza kutekeleza jengo hilo mchana wa leo Ijumaa Novemba 9, 2018.

Ofisa Habari wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji wilaya ya Handeni, Joan Luvena amesema wamekuta moto ni mkubwa hivyo kushindwa kuokoa kitu chochote kutoka katika jengo hilo.

Amesema jitihada za kusafisha eneo hilo ili moto usisambae zaidi zilifanywa kwani majengo ya hoteli hiyo yapo karibu karibu kiasi kwamba hatua za haraka zisipochukuliwa unaweza kusambaa.

"Moto ulikuwa mkubwa sana wahusika walichelewa kutoa taarifa hivyo tumeshindwa kuokoa kitu chochote ila tumeudhibiti hautaendelea kwenye maeneo mengine", amesema Luvena.