In Summary

Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) kimesema kuanzia mwaka 2015 hadi 2018 Tanzania imesajili miradi 905 ya uwekezaji


Dar es Salaam. Jumla ya miradi ya uwekezaji 905 imesajiliwa nchini katika  kipindi cha miaka mitatu ya utawala wa Serikali ya Awamu ya Tano.

Kati ya miradi hiyo, 307 ni ya Watanzania, 319 ya wawekezaji kutoka nje na 277 ni ya ubia kati ya Watanzania na wageni.

Hayo yalisemwa leo na Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), Godfrey Mwambe katika mkutano wake na waandishi wa habari ambao hadi saa 6:00 mchana huu ulikuwa bado unaendelea.

Mwambe alisema miradi yote hiyo ina thamani ya dola za Marekani 13.2 bilioni.

Alisema kati ya miradi hiyo, 478 ni ya viwanda, huku uwekezaji mkubwa ukifanywa na nchi ya China.

Mwambe alisema miradi hiyo ni ile ambayo imefikia vigezo vya kusajiliwa na TIC ambayo kwa mwekezaji wa ndani mtaji wake ni dola za Marekani 100,000 wakati mwekezaji wa nje ni dola 500.000.

Endelea kufuatia Mwananchi wa taarifa zaidi kuhusu TIC na uwekezaji