In Summary
  • Taarifa za Mbunge wa Ukerewe (Chadema), Joseph Mkundi zimeanza kusambaa asubuhi ya leo Oktoba 11, 2018 kwa barua yake kwenda kwa Spika Job Ndugai kuelezea hatua yake ya kujiuzulu na kuhamia CCM

Mwanza. Mbunge wa Ukerewe (Chadema), Joseph Mkundi amejivua uanachama na nyadhifa zake zote na kuhamia Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Ingawa juhudi za kumpata Mkundi kuzungumzia suala hilo hazikupatikana kutokana na simu yake ya kiganjani kutokuwa hewani, Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Ukerewe, Ally Mambile amethibitisha chama hicho kupokea barua ya mbunge huyo kujivua uanachama wa Chadema, kujivua nyadhifa zake na kuhamia CCM.

"Ni kweli tumepokea barua yake tangu jana. Kifupi ni kwamba jimbo la Ukerewe liko wazi na tunaandaa mapokezi maalum kwa ajili yake kwa sababu hili ni jambo kubwa kwa wana Ukerewe," amesema Mambile.