In Summary

Kuongezeka kwa siku hizo mbili kunafanya maonyesho hayo yaliyoanza Juni 28, mwaka huu kudumu kwa siku 18.


Dar es Salaam. Maonyesho ya 42 ya kimataifa ya biashara ya (Sabasaba) yaliyotarajiwa kumalizika Julai 13, yameongezwa siku mbili hivyo yatamalizika Julai 15, mwaka huu. 

Kuongezeka kwa siku hizo mbili kunafanya maonyesho hayo yaliyoanza Juni 28, mwaka huu kudumu kwa siku 18.

Akizungumza na waandishi wa habari  leo Julai 11, katika maonyesho hayo,  Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania(Tantrade), Edwin Rutageruka ametaja sababu ya kuongeza siku za maonesho hayo kuwa ni kutokana na maombi ya wadau.

sababu nyingine ni Naibu Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhandisi Stella Manyanya kuomba muda uongezwe ili kuwapa nafasi zaidi wale ambao hawakupata fursa ya kutembelea maonesho hayo kufanya hivyo.

"Wadau mbalimbali waliomba siku ziongezwe hivyo tumelijadili hilo na Naibu Waziri wetu wa Wizara ya Viwanda tumekubaliana na kuongeza siku mbili mbele ili kuwapa nafasi Watanzania na wadau wengine kupata nafasi ya kutembelea.” amesema

Amefafanua kuwa pamoja na kuongeza siku  maonesho hayo yatafungwa Julai 13 na Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Zanzibar, Balozi Seif Ali  Idd.