In Summary

Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa amezungumzia tukio la kutekwa kwa mfanyabiashara Mohamed Dewji kuwa waliomteka ni Wazungu na watu watatu wanashikiliwa kwa mahojiano


Dar es salaam. Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa amesema waliomteka mfanyabiashara maarufu nchini Mohamed Dewji ‘Mo’ ni Wazungu wawili.

Akizungumza nje ya Hoteli ya Colosseum leo Alhamisi Oktoba 11, 2018 amesema watu watatu wanashikiliwa kuhusika kwa tukio hilo kwa ajili ya mahojiano zaidi.

"Asubuhi ya leo Wazungu wawili walikuwa na gari aina ya Surf. Kulikuwa na magari mawili, moja lilikuwa ndani na lingine nje, gari la ndani liliwasha taa ghafla na lile lililokuwa nje likaingia na kwenda kupaki karibu na gari la MO Dewji lililokuwa limepaki.”

“Na MO akiwa ndani ya gari hilo Wazungu wawili wakatoka na kumbana MO Dewji baada ya kutoka ndani ya gari lake na kisha kumpakia katika gari lao aina ya Surf kisha wakaondoka naye kusikojulikana," amesema Mambosasa.

Hata hivyo, dereva wa Uber amesimulia tukio la kutekwa kwa Mo Dewji akisema alikuwa anakwenda kumshusha abiria katika hoteli hiyo saa 11 asubuhi ndipo alipokutana na tukio hilo.

“Tulikuwa tunakaribia eneo hilo, mara mbele yetu tukaona watu wanne wameshuka kwenye gari dogo wakiwa wamejifunika usoni, wakapiga risasi moja juu, wale askari wa hoteli kila mmoja akakimbia,” anasimulia.

“Waliingia ndani ya hoteli na kutoka na mtu, ambaye nilimjua kuwa ni Mo,” amesimulia dereva huyo ambaye anadai muda mwingi alikuwa amejiinamia kwenye gari kwa hofu.

Inadaiwa waliingia sehemu ya kufanyia mazoezi ‘gym’ na kumkuta hapo huku wakiwaacha watu wengine waliokuwa hapo.

  • Soma zaidi: