In Summary
  • Makonda ametoa agizo hilo leo akiwataka wananchi kuwa huru kufanya hivyo ili kufichua watoa huduma wavivu na wanyanyasaji

Dar es Salaam. Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amesema ‘ruksa’ kwa abiria wa mabasi yaendayo kasi kupiga picha kwenye vituo vya mabasi hayo.

Licha ya katazo la kupiga picha kwenye vituo vya mabasi hayo, Makonda amewataka abiria kuwa huru.

Akizungumza leo alipotembelea kituo cha mabasi cha Kimara, Makonda amesema abiria wapige picha ili kuwafichua watoa huduma wavivu na wanyanyasaji.

"Wewe wakikunyanyasa cha kufanya mrekodi tu kwa simu yako, ukiisambaza kwenye mtandao tutaiona. Mko wengi hawawezi kuwanyang'anya simu zenu zote," amesema.

Amesema ndani ya siku tatu ufumbuzi wa kudumu juu ya kero za usafiri utapatikana.