In Summary

Jogoo huyo alikuwa kivutio kikubwa katika banda la Jeshi la Kujenga Taifa, (JKT) 

Dar es Salaam. Jogoo Silk aliyekuwa akiuzwa Sh 800,000 amenunuliwa kwa Sh 700,000 jana jioni.

Jogoo huyo alikuwa kivutio kikubwa katika banda la Jeshi la Kujenga Taifa, (JKT) katika maonyesho ya kimataifa ya biashara (Sabasaba) yanayoendelea jijini hapa.

Akizungumza na MCL Digital leo Julai 6, mtunzaji na mfugaji wanyama wa banda la JKT, Joshua Buberwa, amesema jogoo huyo ni wa pili kuuzwa.

“Niliwahi kuuza mwingine kabla ya maonyesho haya, kwa Sh 600, 000,” amesema na kuongeza:

“Kesho nitawaleta wengine, ingawa nawatoa mbali, kambi ya Jeshi Kibaha, lakini mwitikio wao utanilazimu kuwaleta."

 Jogoo huyo mwenye asili ya Malaysia, ana umri wa miezi sita, kilo tatu na upekee wake ni manyoya meupe, laini na yaliyojipaga vizuri, tofauti na kuku wengine.