In Summary

Amesema ujenzi wa reli utatoa ajira za moja kwa moja zaidi ya 30,000 na zisizo za moja kwa moja 600,000.


Dar es Salaam. Rais John Magufuli amesema idadi kubwa ya watu nchini haina budi kuendana na maendeleo kwani watu wanapokuwa wengi wanakuwa na sauti na hivyo akawataka Watanzania waendelee kuzaliana.

“Juzi tuliambiwa kwa sasa tumefikia watu milioni 55, watu wanasema kwa nini tunazaliana, mimi nasema tuzaliane tu,” amesema.

Rais Magufuli ameyasema hayo leo Machi 14, wakati wa uzinduzi wa reli ya kisasa (Standard Gauge), Makutupora, Dodoma.

“Lakini idadi hiyo ya watu ni lazima wachape kazi, mfano Denmark ina watu milioni tano lakini wana maendeleo mpaka wanazisaidia nchi nyingine zenye watu milioni 55 kama Tanzania,” amesema.

Amesema ujenzi wa reli utatoa ajira za moja kwa moja zaidi ya 30,000 na zisizo za moja kwa moja 600,000.