In Summary

Baada ya Shirika la Afya Duniani (WHO) kuthibitisha ugonjwa wa Ebola kutua nchini Uganda, Serikali ya Tanzania imewatoa hofu wananchi wake, ikibainisha kuwa imeanza kuchukua tahadhali na kutoa tamko rasmi

Dar es Saalam. Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu amewatoa hofu Watanzania kufuatia Shirika la Afya Duniani (WHO) kuthibitisha ugonjwa wa Ebola kuingia nchini Uganda.

Juni 6, 2019 shirika hilo lilibaini mgonjwa wa Ebola nchini humo Uganda.

Leo Jumatano Juni 12, 2019 kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Twitter, Ummy ameandika ujumbe wa kuwatoa hofu Watanzania, akiwataka kuwa watulivu wakati Serikali ikijipanga kutoa taarifa rasmi.

Amesema Wizara ya Afya imeanza kuchukua tahadhari kukabiliana na ugonjwa huo.