In Summary

Manchester United na Real Madrid zitalazimika kuvunja benki kuwania saini ya beki wa Napoli, aliyewekwa sokoni kwa Pauni90 milioni.


London, England. Miamba ya soka Manchester United na Real Madrid zimeingia vitani kuwania saini ya beki kisiki wa Napoli, Kalidou Koulibaly.

Klabu hizo kila moja inataka saini ya mchezaji huyo katika usajili wa mwezi huu baada ya kucheza kwa kiwango bora msimu uliopita.

Madrid na Man United zinataka beki hodari wa kuzisaidia katika kampeni ya kufanya vyema katika mechi zao msimu uliobaki.

Man United ilikuwa ya kwanza kuwania saini ya beki huyo ikiwa chini ya Kocha Jose Mourinho aliyetaka kumsajili majira ya kiangazi msimu uliopita.

Hata hivyo, klabu hizo zitalazimika kuvunja benki kupata saini ya Koulibaly ambaye  amewekwa sokoni kwa Pauni90 milioni katika usajili wa majira ya kiangazi.

Beki huyo wa kimataifa wa Senegal, amekuwa na kiwango bora katika mashindano ya msimu huu akicheza kwa ustadi katika kikosi cha kwanza cha Napoli.

Mchezaji huyo mwenye miaka 27, amefunga mabao manane na amecheza mechi 141 katika kikosi cha Napoli.