In Summary

Samson Conrad (24), ameuawa baada ya kukatwa na sime shingoni na Kereto Lekoko katika ugomvi wa kudaiana pete

Moshi. Samson Conrad (24), ameuawa akidaiwa kukatwa na sime shingoni na Kereto Lekoko katika ugomvi wa kudaiana pete.

Akizungumza leo Jumatatu Februari 11, 2019, Kamanda wa Polisi Mkoa wa  Kilimanjaro, Hamis Issah amethibitisha kutokea kwa tukio hilo.

Kamanda Isah amesema taarifa za awali zinaonyesha kuwa kabla ya kifo marehemu akiwa na mwanafunzi mwenzake, Andrew Charles, walikuwa katika mazungumzo ya kuuziwa pete na mtuhumiwa huyo.

“Wakati wakiendelea na mazungumzo hawakuelewana na mtuhumiwa akitaka kupatiwa fedha yake, na alichomoa sime na kumjeruhi  marehemu shingoni. Alivuja damu nyingi na amefariki dunia,”amesema Kamanda Issah