In Summary

Baba huyo amesema kwamba mtoto ni wake na hata alipoumwa alitumia bima kumtibu.


Dar es Salaam. Peter, anayedai kuwa ndiye baba wa mtoto wa Muna amefunguka na kusisitiza kuwa yeye ndio baba halali wa mtoto huyo huku akitishia kususia msiba huo kama utapelekwa Mbezi.

Akizungumza na MCL Digital, Peter, amesema toka mwaka jana mtoto huyo aitwaye Patrick alipokuwa anaumwa alikuwa anamhudumia mwenyewe kupitia bima ya Afya ya Jubilee na alikuwa anakatwa ofisini kwake.

Peter amesema yeye ni mume wa ndoa wa Rose Alphonse, wengi wamezoea kumuita 'Muna Love ', wamefunga ndoa mwaka 2010 na walijaaliwa kumzaa Patrick mwaka 2011.

Peter pia amesema hakuwahi kuachana na Muna ila alipoondoka nyumbani walipokuwa wanaishi Mwananyamala, ndipo akaanza kuona Caston ambaye anadai Patrick ni mwanae, akimposti katika mitandao.

Akifafanua zaidi Peter anasema baada ya kumuona Caston anamposti Patrick mitandaoni alimuuliza Muna na ndipo ugomvi ulipoanzia na kuondoka nyumbani.

"Mimi kwanza huyo Caston anayedai kuwa Patrick ni mwanae nimeanza kumfahamu kipindi Patrick amefikisha miaka mitano, tena nilistuka baada ya kuona amemposti katika mitandao na kusema ni wake,’’ amefunguka Peter.

"Kwanza ni mtu gani ambaye hushituki na kuona cheti cha kuzaliwa cha mtoto kimeandikwa Peter Zakaria Komu, hadi utangaze ni wako? Na hili suala hajaanza leo, toka mimi namuhangaikia mtoto akiwa hospitali mwaka jana.” Amesema Peter.

Katika kushikilia msimamo wa kuwa yeye ndiye baba wa Patrick, Peter amedai kuwa kama Muna atalazimisha msiba uwe Mbezi Jogoo basi yeye hatahusika na mazishi, ila kama utaendelea kuwa nyumbani kwake Mwananyamala basi ataubeba msiba yeye kama baba bila michango ya watu wanaochangisha.

Soma Zaidi: