In Summary

Ni katika mpango  wa kuendelea kuboresha mikakati yake ya kibiashara, kiutendaji na kiuendeshaji

Dar es Salaam. Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) lintaanza safari za kwenda China kwa kutumia Dreamliner kuanzia Februari mwakani.

Hayo yamesemwa na meneja masoko wa kampuni hiyo, Edward Nkwabi alipokuwa akizungumzia mikakati ya kuongeza watalii nchini.

Alisema ndege hiyo ina uwezo wa kubeba abiria 266 pamoja na mzigo tani 15 itakuwa ikifanya safari mara tatu kwa wiki.

“Tumelenga kuanza safari za China kwa kuwa ni nchi ya biashara na yenye watalii wengi, tutakuwa tukifanya safari kila Jumnne, Alhamisi na Jumamosi,” amesema Nkwabi.

Amesema safari hizo zitaanzia jijini Dar es Salaam kwenda moja kwa moja katika Mji wa Guangzhou kwa nauli ya Dola 650 na Bangkok kwa Dola 700.

Katika mpango huo, ATCL inashirikiana na Bodi ya Utalii Tanzania (TTB). Mwenyekiti wa bodi hiyo, Jaji mstaafu Thomas Mihayo amesema wanashiki maonyesho ya utalii yanayoandaliwa nchini humo.

“Bodi inashirikiana na ubalozi wetu na Shirika la Ndege Tanzania kutangaza utalii katika miji mbalimbali ya China,” alisema Mihayo.