In Summary

Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) leo Alhamisi imetoa tahadhari ya siku tano ya kuwepo kwa upepo mkali na mawimbi makubwa katika maeneo ya Ziwa Nyasa.

Dar es Salaam.  Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imetoa tahadhari ya siku tano ya kuwepo kwa upepo mkali na mawimbi makubwa katika maeneo ya Ziwa Nyasa.

Taarifa ya TMA iliyotolewa leo Alhamisi Novemba 8, 2018 imesema kuanzia leo hadi Novemba 11, 2018 kutakuwepo na upepo mkali na mawimbi makubwa katika maeneo hayo.

TMA imesema kuna uwezekano wa kutokea kiwango cha athari ikiwemo baadhi ya shughuli za uvuvi na usafiri baharini kuwa mgumu.

Imesema athari nyingine ni kupeperushwa kwa takataka mitaani na kuanguka kwa majani na matawi madogomadogo ya miti.

TMA imewashauri watumiaji wa bahari na wakazi wa maeneo hayo kuchukua tahadhari na hatua stahiki huku mamlaka hiyo ikiendelea kufuatilia hali hii na itatoa mrejesho kila itakapobidi.