In Summary

Taarifa iliyotolewa leo Alhamisi na Katibu Mkuu wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dk Faraji Mnyepe imesema Rais Magufuli ametengua uteuzi wa balozi wa Tanzania nchini Canada, Alphayo Kidata.

Dar es Salaam. Rais John Magufuli ametengua uteuzi na kumrejesha nchini Tanzania aliyekuwa Balozi wa Tanzania, Canada, Alphayo Kidata.

Taarifa iliyotolewa leo jioni Alhamisi na Katibu Mkuu wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dk Faraji Mnyepe imesema uamuzi huo umeanza Novemba 5, 2018.

Dk Mnyepe amesema Kidata ameondolewa hadhi ya Ubalozi.

Habari zinazohusiana: