In Summary

Marehemu Elia na Shilole wamefanikiwa kupata mtoto mmoja wa kike aitwaje  Joyce Godfrey  mwenye umri wa miaka 14 ambaye pia ndio mtoto wa kwanza wa Shilole .

Dar es Salaam. Mzazi mwenzake na msanii wa filamu nchini Zuwena Mohammed maarufu kama Shilole,  Makala Elia, amefariki dunia ghafla huko Igunga mkoani Tabora. Elia ndiye  baba wa mtoto wa kwanza wa Shilole.

Akizungumza na MCL Digital, leo Juni 6 Shilole amesema, mzazi mwenzie amefariki ghafla baada ya kutoka kwenye starehe usiku wa kuamkia leo na alikuwa haumwi.

"Elia alikuwa mzima wa afya wala hakuwa anaumwa, mara ya mwisho kuwasiliana naye ilikuwa ni miezi miwili iliyopita, yaani kiukweli nimesikitishwa sana na kifo chake na hivi ninavyokwambia leo napanda gari kwenda Igunga kwa ajili ya mazishi," amesema Shilole.

Marehemu Elia na Shilole wamefanikiwa kupata mtoto mmoja wa kike aitwaje  Joyce Godfrey  mwenye umri wa miaka 14 ambaye pia ndio mtoto wa kwanza wa Shilole .