In Summary

Chanzo cha mauaji hayo inadaiwa ni ugomvi wa kifamilia

 

Wananchi wa kijiji cha Butahyaibega Wilaya ya Bukoba wameendesha msako usiku kucha wakimtafuta mtuhumiwa wa mauaji ya watoto wake pacha.

Mtuhumiwa huyo, anadaiwa kuwaua kwa kuwachinja pacha hao, usiku wa kuamkia siku ya Jumapili.

Mwenyekiti wa Kitongoji cha Bulambizi,Dickson Barongo amesema usiku kucha wamekesha wakiendesha msako maeneo yote ya kijiji na kufanya ukaguzi maporini wakimsaka mtuhumiwa.

"Tumezingira maeneo yote yanayoingia na kutoka kwenye kijiji msako umefanyika usiku kucha wananchi wameungana kwa pamoja kumtafuta mtuhumiwa mpaka atakapopatikana tuna uhakika hajatoka nje ya kijiji cha Butahyaibega,"amesema Barongo

Chanzo cha mauaji hayo inadaiwa ni ugomvi wa kifamilia.

 Ofisa Mnadhimu wa Polisi Mkoa wa Kagera, Isaac Msengi amesema ufafanuzi wa suala la mauaji hayo utafanywa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kagera, Augustine Ollomi.