In Summary
  • Sanga ambaye pia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Ligi Kuu Bara (TPLB), alisema Yanga ina kampuni halali ambayo ilishapitishwa katika mikutano ya klabu yao na sasa kwa kuwa serikali imekubali timu hizo zibadilike, basi nao wataanza mambo.

Kaimu Mwenyekiti wa Yanga, Mhandisi Clement Sanga amewaambia Simba sio wa kwanza kuanzisha mfumo huo, kwani klabu yake ilikuwa ya kwanza na mpaka sasa kampuni hiyo ipo ingawa kuna mambo machache yalitakiwa kufanyiwa kazi.

Sanga ambaye pia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Ligi Kuu Bara (TPLB), alisema Yanga ina kampuni halali ambayo ilishapitishwa katika mikutano ya klabu yao na sasa kwa kuwa serikali imekubali timu hizo zibadilike, basi nao wataanza mambo.

Alisema Yanga anayoingoza yeye itarudisha mipango hiyo kwa kufuata kile ambacho serikali inataka kukifanya kwa kuhakikisha utaratibu unafuatwa kwa usahihi. Alidokeza Kamati ya Utendaji ya Yanga itakutana Desemba 13 kujadili.