In Summary
  • wanasoka bora wa dunia wa zamani Mliberia huyo amegombea urais nchini humo na matokeo bado yanakamilishwa kabla ya kutangazwa rasmi.

London, England. Kocha wa Arsenal, Arsene Wenger amempongeza George Weah kwenye akaunti yake ya Twetter akiamini ameshinda uchaguzi Mkuu nchini Liberia huku matokeo rasmi yakiwa bado hayajatangazwa.

Wenger aliuvaa mkenge huo baada ya kusoma taarifa kwenye mtandao kuhusu ushindi wa uchaguzi wa Rais, nchini Liberia ambapo taarifa zinaeleza kwamba kazi ya kukamilisha matokeo ya mwisho bado inaendelea.

Kocha huyo aliandika, “Ninapenda kukupongeza mmoja wa wachezaji wa zamani ambaye umekuwa Rais wa Liberia, George Weah.

Hii sio mara ya kwanza kwa mchezaji wa zamani kuwa rais wa nchi na umefanya vyema George Weah…”