In Summary
  • Wakongwe wa Yanga washauri hata wanachama wa Yanga waelimishwe wasizuie mabadiliko.

Mabadiliko ya Simba yamewagusa watani zao Yanga, ambapo nyota wa zamani wa timu hiyo pamoja na watendaji wengine wameipa tano Simba na kuwaambia kuwa mabadiliko hayo yatawabeba.

Katibu Mkuu wa zamani wa Yanga, Lawrence Mwalusako alisema kama kuna jambo la maana Simba wamefanya ni kuikabidhi timu hiyo kwa wenye fedha.

"Hili jambo si la kishabiki, linataka elimu ya hali ya juu ili wanachama walielewe. Mfumo wa hisa ni wa kisasa, unasaidia kupunguza baadhi ya kero zisizo na sababu, mfano mzuri namna wanavyochangishana wanachama wa Yanga na Simba, hayo yatapungua badala yake, kutakuwa na mpango madhubuti," alisema.

Katibu mwenezi wa zamani wa Yanga, Abdul Sauko alisema kuingia kwenye hisa ni kitu sahihi kwa watani zao hao.

"Licha ya kwamba Simba hawajafikia mwafaka, naona wapo sehemu nzuri. Wanachama wa Yanga waelimishwe pia juu ya mfumo huo ambao utafanya klabu iwe ya kisasa," alisema Sauko.