In Summary
  • Katibu mkuu wa klabu hiyo, Charles Boniface Mkwasa alisema wanaendelea kusajili kwa kufuata orodha ya mahitaji ya kocha George Lwandamina .

 Baada  ya Yanga kumnasa  Ibrahim Ajib, klabu hiyo imeibuka na kusema mambo  bado na imewataka wanachama wake kuendelea kusubiri  wachezaji wengine itakaowasajili.

Katibu mkuu wa klabu hiyo, Charles Boniface Mkwasa alisema wanaendelea kusajili kwa kufuata orodha ya mahitaji ya kocha George Lwandamina .

“Usajili bado unaendelea, ila hatuwezi kuweka majina wazi ya wachezaji  gani  tunaowahitaji, kuhusu Abdallah Haji Shaibu ‘Ninja’ mwalimu alimuona kwenye  mashindano ya Mapinduzi, ndiyo maana tumemsajili.

“Kulikuwa na maswali mengi kuhusu usajili wake, tunajua nini tunafanya tena niweke wazi kuwa usajili wetu unaenda kwa mpangilio maalum,” alisema Mkwasa.