In Summary
  • Beki huyo wa kimataifa wa Ivory Coast amekuwa na mchango mkubwa katika mafanikio ya safu ya ulinzi ya Man United msimu huu.

London, England. Beki Eric Bailly ndiye nguzo ya Manchester United iliyoziba vizuri pengo la Steve Bruce na Nemanja Vidic, kwa mujibu wa mkongwe wa Old Trafford, Gary Pallister.

Beki mwenye kipaji katika ukuta wa Man United ilikuwa ni kitu adimu tangu kuondoka kwa Alex Ferguson, lakini kupata beki aliyekamilika si jambo rahisi.

Kwa sasa ukuta wa Old Trafford una mabeki kama Chris Smalling, Daley Blind na Victor Lindelof wote wanauwezo wa kuchezea mpira awali walikuwepo Rio Ferdinand, Laurent Blanc na Jonny Evans.

Lakini usajili wa msimu huu wa Bailly umeongeza kitu cha kipekee katika ngome hiyo na kuwaweka wengine katika mazingira magumu kama Phil Jones.

Kuelekea mchezo kati ya Man United dhidi ya Liverpool, Pallister ameiambia betsafe.com: “Kumekuwa na maswali mengi kuhusu Phil Jones katika miaka iliyopita kutokana na kusumbuliwa kwa majeruhi na kiwango chake na amekuwa katika changamoto nyingi mwaka huu.

“Bailly anapenda kulinda langome yake kama ilivyokuwa kwa Vidic au Steve Bruce, anajituma vilivyo.

“Liverpool ni kipimo sahihi, cha safu yetu ya ulinzi kwa sababu hii mechi ni tofauti kabisa."