In Summary
  • Mshambuliaji huyo wa zamani wa Yanga alicheza soka la kulipwa nchini Angola

Dar es Salaam. Mshambuliaji wa zamani wa  Yanga na Taifa Stars, Said Maulidi 'SMG' amesema mchezaji anayezingatia miiko ya soka na kujituma mafanikio ni wazi kwake.

SMG alisema kwa sasa kwenye soka fursa zipo nyingi tofauti na zamani ambapo wengi wao walichezea mapenzi na vipaji walionyesha.

SMG anawashauri wachezaji wasijibweteke na kipato wanachopata bali kiendane na kazi zao uwanjani anazodai ndizo zitakazowafanya wafike kwenye nyanja mbalimbali.

"Waige kwa mwenzao Mbwana Samatta huyo fursa zake zipo wazi lasivyo kazi zao zitaendelea kudharaulika kila iitwapo leo,"anasema.