In Summary

Italia imeshindwa kufuzu kwa Kombe la Dunia kwa mara ya kwanza tangu 1958

Milan, Italia. Kipa Gianluigi Buffon alitokwa na machozi huku akisema sitaki kujionea huruma mwenyewe bali kwa soka la Italia kwa ujumla.

Italia imepata pigo kwa kushindwa kuitoa Sweden na sasa wameshindwa kufuzu kwa Kombe la Dunia kwa mara ya kwanza tangu 1958, kutolewa huko kumekuwa ni pigo kubwa kipa Buffon, ambaye alipanga kustaafu mwisho wa msimu huu.

Bao la Jakob Johansson katika mchezo wa kwanza ulikuwa ni mlima mkubwa kwenye Uwanja wa San Siro kwa vijana wa Gian Piero Ventura kushindwa kuifunga Sweden.

"Siyo pigo la kwangu mwenyewe, lakini ni pigo kwa soka la Italia," alisema Buffon, baada ya filimbi ya mwisho.

"Tumeshindwa katika kitu kilichoonyesha kuna jambo alipo sawa katika jamii. Najutia kumaliza kwa namna hii, si kwa sababu muda wangu umepita."

Alisisitiza kufuzu kwa mashindano haya haikuwa jambo rahisi,lakini hakuna sababu ya kwepa lawama.

"Kwa wale wanaocheza soka wanajua jinsi gani mechi hii ilivyokuwa ngumu. Tulishindwa kuonyesha ubora wetu. Tulipoteza umakini katika kutumia nafasi za kufunga," alisisitiza Buffon.