In Summary
  • Awali, utata uliiibuka kuhusu ushiriki wa Simbu  kwenye mbio hizo tofauti za dunia na majeshi.

 Mwanariadha maarufu nchini, Alphonce Felix Simbu atashiriki mbio za dunia na majeshi kwa mwezi Agosti.

Awali, utata uliiibuka kuhusu ushiriki wa Simbu  kwenye mbio hizo tofauti za dunia na majeshi.

Simbu ni miongoni mwa wanariadha waliofuzu kushiriki mbio za dunia lakini pia yuko kwenye kikosi cha Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) kitakachoshiriki mashindano ya Majeshi ya Afrika Mashariki.

Simbu ambaye ni mwajiriwa wa JKTalilazimika kuamua mbio zipi atashiriki,. kwani zote zinafanyika Agosti.

"Kwenye mbio za dunia, nitakimbia marathon (km 42),  hizi ni mbio kubwa na bila shaka hata waajili wangu watapenda kuona nashinda huko kwani ni kubwa zenye rekodi, lakini pia za majeshi zina umuhimu.

"Nimefuatilia ratiba inaonyesha kwenye mbio za dunia, marathoni zinafanyika mwanzoni, hivyo nitakwenda nitakimbia kisha nitatejea kwenye timu yetu itakayoshiriki mashindano ya majeshi.

"Kule kwenye majeshi nakimbia mbio za kilomita10, ni umbali mdogo kwangu ni kama nafanya 'warm up' (mazoezi)…" alisema.