In Summary
  • Mashambuliaji huyo anahusishwa na kutaka kuondoka Arsenal tangu mwanzo wa msimu huu

 Mshambuliaji Alexis Sanchez yuko tayari kwa kutoa busu la kheri kwa mashabiki wa Arsenal kwa kukamilisha uhamisho wake wa pauni 25milioni na kujiunga na Manchester City mwezi huu.

Bosi wa Etihad, Pep Guardiola ameweka wazi nia yake ya kumtaka nyota huyo wa Arsenal anayetaka kuondoka katika klabu hiyo.

Sanchez  ameweka bayana nia ya kuondoa Arsenal licha ya kukumbana na kikwazo kutoka kwa bosi wake Arsene Wenger.

Man City inataka kujaribu bahati kwa mara ya mwisho baada ya jaribio lake kugonga mwamba mara kadhaa licha ya kuweka mezani Puani 35 milioni.

Mchezaji huyo wa kimataifa wa Chile amegoma kutia saini mkataba mpya na endapo klabu hiyo itaendelea kumuwekea ngumu msimu ujao wa majira ya kiangazi ataondoka akiwa mchezaji huru.

Sanchez anataka kucheza pembeni ya kocha Pep Guardiola, anayemtaka muda mrefu kutokana na ubora wa kiwango chake uwanjani.

Man City imeweka ngumu kuongeza dau kwa kuwa ina uhakika itamsajili Sanchez akiwa huru majira ya kiangazi baada ya kuonyesha mapenzi na klabu hiyo.

Guadiola amemtaka kwa nguvu Sanchez kuimarisha safu ya ushambuliaji baada ya kumkosa kinda Gabriel Jesus ambaye atakuwa nje ya uwanja wiki tatu akiuguza jeraha la goti.

Kocha huyo amebakiwa na mshambuliaji mmoja Muargentina Sergio ‘Kun’ Aguero katika kikosi hicho kutoka Makao Makuu Etihad.

Wakati Man City ikipambana kupata saini ya mshambuliaji huyo, Arsenal imeongeza kasi ya kumsajili Thomas Lemar wa Monaco.