In Summary
  • Tangu 2009 ni Messi na Ronaldo pekee waliofanikiwa kunyakuwa tuzo hiyo

Madrid, Hispania. Wasomaji wa gazeti la Marca amemtaja mshambuliaji Cristiano Ronaldo kuwa ndiye mshinda tuzo ya Ballon d'Or kwa mujibu wa kura walizopiga.

Orodha ya wachezaji wanaowania tuzo hiyo ilitangazwa Jumatatu na mashabiki kuamua kupiga kura ya mchezaji gani atwaa tuzo hiyo mwaka huu.

Asilimia 64 ya kura za wasomaji zinaamini Ronaldo anastahili kushindi zawadi hiyo kwa mwaka wa pili mfululizo.

Nafasi ya pili imechukuliwa na mshambuliaji wa Barcelona, Lionel Messi aliyepata asilimia 26, ya kura huku Isco akiwa wa tatu kwa kupata asilimia mbili ya kura hizo.

Walipopata asilimia moja ni pamoja na Sergio Ramos, Neymar, Luka Modric, Toni Kroos na Kylian Mbappe katika kura hizo za wasomajia zaidi 5,500 walioshiriki.