RAYON Sports imethibitisha kwamba Hamad Ndikumana ambaye ni mzazi  mwenza wa msanii wa filamu wa Tanzania, Irene Uwoya amefariki dunia ghafla leo Jumatano saa kumi alfajiri, nyumbani kwake Nyamiramo, Jijini Kigali Rwanda.

Gakwaya Olivier ambaye ni Afisa Habari wa Rayon ya Rwanda, amesema muda mfupi uliopita kwamba Ndikumana ambaye alikuwa kocha wao msaidizi amefariki kwa kile kinachosadikiwa kuwa ni ugonjwa wa moyo.

“Alisikia maumivu makali kifuani akaomba soda ya baridi wakamletea na alipomaliza kunywa tu kidogo akatapika na akaishiwa pumzi na ndipo akakata kauli,”alisema Olivier na kuongeza kwamba bado wanasubiri uchunguzi wa kina wa kitabibu.

Ndikumana alikuwa mzazi mwenza wa Uwoya ingawa katika siku za hivikaribuni iliripotiwa kwamba Uwoya aliolewa na msanii wa kizazi kipya, Dogo Janja.