In Summary
  • Simba ni bingwa wa Ligi Kuu bara mara 18 mara ya mwisho kuchukua ubingwa huo ni miaka minne iliyopita.

Dar es Salaam. Winga wa zamani wa Simba, Ulimboka Mwakingwe, amesema kocha Joseph Omog na msaidizi wake Jaskson Mayanja wataachwa huru bila kuingilia basi milango ya ubingwa ni wazi.

Simba ilitwaa ubingwa wa Ligi Kuu Bara mara ya mwisho mwaka 2012, baada ya kuifunga Yanga mabao 5-0 katika mchezo wa mwisho.

Ulimboka alisema anayeipenda Simba kwa dhati ana hamu ya kuona taji la ubingwa linatua Msimbazi, akisisitiza kitu pekee cha kufanikisha hilo ni kuepuka muingilio wa majukumu.

"Binafsi nina imani na Omog na kikosi ni kizuri, kinachotakiwa tuache taaluma zao zifanye kazi, kocha afundishe na wachezaji wafanye kazi yao uwanjani, hapo tutaona mafanikio,"alisema

"Tukitathimini kitu gani kimetukwamisha miaka minne iliyopita ni rahisi kufikia pointi la sivyo kama hatujui tulipoangukia inaweza kuwa maumivu mapya, ila tusifike huko,"alisisitiza Ulimboka.