In Summary
  • Mhina alisema ingawa amepewa mikoba hivi karibuni, lakini rekodi zinaonyesha Majimaji haijawahi kufika raundi ya tatu ya Kombe la FA.

Mbeya. Kocha wa Majimaji ya Songea Peter Mhina amesema atalipa kisasi dhidi ya Ruvu Shooting katika mechi ya Kombe la Shirikisho (FA) inayoratajiwa kuchezwa Januari 31.Majimaji inayojifua kwenye Uwanja wa Majimaji, ilichapwa na Ruvu Shooting mabao 2-1 katika mechi Ligi Kuu Tanzania Bara. Mhina alisema ingawa amepewa mikoba hivi karibuni, lakini rekodi zinaonyesha Majimaji haijawahi kufika raundi ya tatu ya Kombe la FA.“Nataka niwaaminishe wanasongea niko hapa kwa ajili ya kuipaisha Majimaji kwenye FA, Ligi Kuu na kuhakikisha tunamaliza katika nafasi nzuri. Niliwasoma wachezaji tulipokutana nao kwenye mechi ya ligi mbinu na mfumo wao ninao hawanipi shida,’’alisema Mhina. (Justa Mussa)