In Summary

Agomea kufuta kesi iliyofungua mahakamani mwaka huu.

LICHA ya serikali kuridhia wawekezaji ndani ya klabu za soka za wanachama ikielekeza wapewe asilimia 49 na zilizosalia ziwe za wanachama, aliyekuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini wa Simba, Hamis Kilomoni amegoma kufuta kesi mahakamani akidai bado kuna chenga chenga katika mabadiliko ya Simba.

Hivi karibuni Serikali kupitia Wizara ya Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo iliitaka Simba kwenda kwenye mabadiliko kwa sharti la kumpa mwekezaji asilimia 49 ya hisa na asilimia 51 zibaki kwa wanachama.

Licha ya Kilomoni kupata alichokihitaji, bado amesisitiza hafuti kesi hadi pale atakaporidhika na mchakato wa mwekezaji Mo Dewji aliyepewa Simba uende sawa.

"Bado mapema mno kufuta kesi, sababu hawa jamaa (akimaanisha viongozi wa Simba) naona wanakomalia asilimia 50 kwa 50 wakati serikali ilishasema 49-51, siwezi kufuta kesi wakati naona chenga chenga.