In Summary
  • Kili Stars inayonolewa na Kocha Ammy Ninje ilianza michuano hiyo kwa sare tasa na Libya katika mechi za Kundi A, hali inayoifanya lazima ishinde kesho Alhamisi kwenye Uwanja wa wa Kenyatta, mjini Machakos.

TIMU ya soka ya Tanzania Bara, Kilimanjaro Stars kesho Alhamisi itakuwa na kibarua kigumu katika michuano ya Kombe la Chalenji wakati watakapokabiliana na ndugu zao wa Zanzibar Heroes, ili kuamua hatima yao ya kutinga nusu fainali.

Kili Stars inayonolewa na Kocha Ammy Ninje ilianza michuano hiyo kwa sare tasa na Libya katika mechi za Kundi A, hali inayoifanya lazima ishinde kesho Alhamisi kwenye Uwanja wa wa Kenyatta, mjini Machakos.

Zanzibar Heroes ilianza kwa kishindo michuano hiyo juzi kwa kuichapa Rwanda mabao 3-1 na kuifanya ishike nafasi ya pili nyuma ya wenyeji wao Kenya wanaoongoza msimamo wa kundi lao wakiwa na alama 4.