In Summary
  • Simba imeondolewa katika mashindano ya Kombe la Mapinduzi

 Nyota wa Simba, Shiza Kichuya, Jonas Mkude, Mwinyi Kazimoto na Nicholas Gyan wameonyesha kitendo cha utovu wa nidhamu wakati wa mchezo wao dhidi ya URA.

Katika mchezo huo ambao Simba ilifungwa bao 1-0 na URA na kuondolewa mashindano ulishudia wachezaji wa Kichuya, Mkude na Gyan wakijiondoa katika benchi la timu hiyo baada ya kutolea.

Kichuya alitolewa kipindi cha kwanza alikaa kwenye benchi la wachezaji wa akiba huku akikataa kupewa mkononi na kocha wake Djuma Masoud na kugomea kupewa maji ya kunywa na daktari wa Simba, Yassin Gembe.

Walipoenda vyumbani kupata maelekezo wakati wa mapumziko walitolewa Kazimoto, Mkude na Gyan ambao hawakurudi kwenye benchi na kubaki vyumbani baadae wanatoka na kukaa kwa mashabiki.

Wachezaji hao walipotoka nafasi zao zilichukuliwa na Yusuph Mlipili,  Said Ndemla na James Kotei na Mohammed Ibrahim 'MO'.

Djuma alipoulizwa Kuhusu kutokurudi kwa wachezaji hao kwenye benchi alisema kuwa walipata majeruhi na walikuwa wakitibiwa.

"Walipata majeraha ya misuli na walikuwa wanapata matibabu," alisema Djuma.