In Summary


        Mwanza. Klabu ya Kagera Sugar imesema kuwa haitaki mzaha katika mechi zake na imetamba lazima iitungue Njombe Mji kwenye mchezo Ligi Kuu Tanzania Bara.Kagera Sugar inayonolewa na kocha mkuu Mecky Maxime (pichani) ipo nafasi ya 12 kwa pointi 12, inatarajia kujitupa uwanjani Jumatatu ijayo kuikabili Njombe Mji kwenye Uwanja wa Sabasaba mkoani humo.Kocha msaidizi Ally Jangalu alisema timu hiyo imewasili mkoani humo mapema kuzoea hali ya hewa ikiwa ni sehemu ya mkakati ya kuvuna pointi tatu.

(Masoud Masasi)