In Summary
  • Kocha huyo anakuwa miongoni mwa makocha bora wanaolipwa vizuri duniani.

London, England. Uongozi wa Manchester United umeamua kufanya kweli baada ya kutangaza kumuongezea mkataba wa miaka mitano kocha wake, Jose Mourinho kwa dau la Paui 65 milioni.

Uamuzi huo umekuja baada ya kikosi hicho cha Manchester United kuanza vyema msimu huu kwenye mechi za Ligi Kuu.

Ushindi mfululizo wa kocha Mourinho umewashawishi mabosi hao jambo ambalo limewafanya wafunguke kuhusu kumuongezea mkataba huo mnono.

Hatua hiyo imepokewa kwa furaha na kocha Jose Mourinho ambaye yupo tayari kusaini mkataba huo mpya unaompa nafasi kukitumikia kikosi hicho kwa muda mrefu zaidi.

Mourinho mwenye miaka 54 anatajwa kuwa miongoni mwa makaocha bora duniani wanaolipwa vyema akifuatia kwa Pep Guardiola ambaye anapokea mshahara wa Pauni 250,000 kwa wiki.

Hata hivyo mshahara wa Mourinho unatajwa kuendelea kuwa uleule lakini akifanikiwa kutwaa mataji dau lake linaweza kubadilika.