In Summary

Jose Mourinho yupo tayari kuachana na beki wa Kitaliano, Matteo Darmian, mwishoni mwa msimu.

MANCHESTER United imeripotiwa kuwa katika mazungumzo mazuri na Valencia kwa ajili ya kumchukua beki, Jose Gaya, wakati huu kocha, Jose Mourinho akiwa tayari kuachana na beki wa Kitaliano, Matteo Darmian, mwishoni mwa msimu.

Gaya ambaye pia amekuwa akifuatiliwa na Chelsea na Arsenal, ameichezea Valencia mechi 106 tangu alipotinga katika kikosi cha kwanza klabuni hapo mwaka 2012 na sasa Manchester United inataka kupiga bao.