In Summary
  • Dante, anaeleza jinsi ambavyo Yanga, wanajua kushindana kwamba kila mchezaji anapenda kutambulika na wadau wa soka nchini kwamba ana kitu cha tofauti kuliko mwingine.

 Kumbe usajili unaoendelea kwa sasa unawafanya wachezaji wasilale usingizi, sikia alichozungumza beki wa Yanga, Andrew Vicent 'Dante' kuwa yupo makini kujua nyota yupi ataongezwa kwenye nafasi yake kisha aujue jinsi ya kujipanga.

"Unapoletewa mpinzani wako lazima ujue uwezo wake kisha unaanza kujifua kujua ni jinsi gani utapata namba,hivyo kuwa makini na usajili si kitu kibaya,"anasema

Dante, anaeleza jinsi ambavyo Yanga, wanajua kushindana kwamba kila mchezaji anapenda kutambulika na wadau wa soka nchini kwamba ana kitu cha tofauti kuliko mwingine.

"Nafurahia ushindani ambao unaweza kunifikisha kwenye ndoto yangu na plani yangu kila msimu natamani kuwa na hatua moja zaidi,"anasema