In Summary

Ratiba ya hatua ya mtoano ya Ligi ya Mabingwa itapangwa Jumatatu ijayo

Madrid, Hispania. Wakati ratiba ya mtoano wa Ligi ya Mabingwa ikitarajiwa kupangwa Jumatatu ijayo, watabiri wanaona Chelsea itapangwa na Barcelona, wakati Real Madrid au Sevilla uwenda wakapangwa na miamba ya Italia, Roma.

Baada ya Atletico Madrid kushuka hadi Europa Ligi, kumefanya Hispania kuwa na timu tatu katika hatua ya 16 bora.

Hiyo ndiyo hatua muhimu zaidi katika mashindano hayo wakati vinara wa makundi watakapopangwa na washindi wa pili kuamua timu zitakazofuzu kwa robo fainali, hata hivyo klabu za nchi moja hazitakuna zenyewe katika hatua hii.

Barcelona imefuzu kama kinara wa kundi wakati Real na Sevilla wenyewe wakiwa katika nafasi ya pili katika makundi yao.

Ratiba hiyo ya Jumatatu imeongeza hamasa kwa jinsi timu hizo zitakavyokuwa tayari kuwajua wapinzani wao.
Inaonyesha katika timu ambazo zinaweza kupangwa na Barcelona inayopewa nafasi kubwa kwa asilimia 40 ni Chelsea.

Real Madrid na Sevilla wenye wanamtihani zaidi kwa sababu hawana timu ambao ina asilimia kubwa ya kucheza nazao isipokuwa Roma tu kwa asilimia 19.

Kwa mazingira hayo pia kuna uwezekano wa Manchester United na Manchester City zote kwa asilimia 18 zinawezwa kupangwa dhidi ya mabingwa watetezi, Real Madrid.