In Summary
  • Barcelona inamtaka Coutinho ili kuziba pengo la Neymar aliyetimkia PSG msimu huu

London, England. BARCELONA ipo tayari kumnunua kiungo wa Liverpool, Philippe Coutinho katika uhamisho wa Januaria baada ya kushindwa wakati wa dirisha kubwa la usajili.

Miamba hiyo ya La Liga walishindwa kufikia dau lake katika siku ya mwisho ya usajili, wakati Liverpool lipotangaza inataka pauni180milioni kwa ajili ya Coutinho "Little Magician".

Kocha wa Liverpool, Jurgen Klopp alikataa dau la pauni 138 milioni walilotaka kutoa Barcelona jambo lililomfanya mkurungezi wa Barca, Albert Soler kudai bei wanayotaka Liverpool iliwafanya washindwe.

Soler alidai kuwa: "Baada ya wiki ya majadiliano, jana Liverpool alituambia tuwalipe pauni180milioni kwa ajili ya mchezaji huyo. Hatutoweza kuiweka klabu katika matatizo.

"Wakati wote tunafanya kazi kwa malengo, hatutaki kuingiza klabu katika matatizo kwa sababu hii inamilikiwa na wanachama.

"Uwezo wa PSG kuja na kumnunu Neymar kwa euro 222milioni haikuwa tatizo kwa sababu kila moja anajua ni wapi fedha za klabu hiyo zinatoka.

Lakini sasa, Barcelona inasema ipo tayari kumnunua nyota huyo wa Brazil kwa mujbu wa mkurungezi mtendaji, Oscar Grau.

Grau alidai kuwa: "Tupo tayari kumnunua Coutinho wakati wa usajili wa dirisha dogo, au mchezaji yeyote anayetakiwa na benchi la ufundi.

"Jambo la muhimu ni kujiandaa sisi wenyewe, kama atakuja basi tunatakiwa kujua nina ataondoka pia.