London, England. Makocha wanaozinoa timu zinazopewa nafasi ya kutwaa Kombe la Dunia, wameanza kurushiana vijembe zikiwa zimebaki siku mbili kabla ya kuanza michuano hiyo.

Timu za Brazil, Ufaransa na mabingwa watetezi Ujerumani, wanapewa nafasi ya kutwaa ubingwa katika fainali hizo zilizopangwa kuanza Juni 14 nchini Russia.

Makocha wa timu hizo kila mmoja amevutia upande wake akitambia wachezaji nyota wanaoweza ‘kumtoa’ katika fainali hizo.

Brazil

Brazil ilikuwa timu ya kwanza kukata tiketi ya kwenda Russia, lakini jinamizi la kunyukwa mabao 7-1 na Ujerumani katika fainali za mwaka 2014 bado linaiandama.

Tegemeo kubwa la Brazil katika fainali hizo ni uwepo wa safu ya ushambuliaji ambayo inaongozwa na Gabriel Jesus, Phillipe Coutinho na Neymar.

“Brazil ni timu inayopewa nafasi kubwa ya kutwaa ubingwa, katika kiwango cha soka naamini tumemitiza wajibu wetu kwa kiwango cha juu ukijumlisha na matokeo yetu…tuna umoja na tutashinda,” alisema kocha wa timu hiyo Tite.

Ufaransa

Kocha Didier Deschamps anakwenda Russia na timu yenye damu mchanganyiko wakiwemo mastaa wengi wanaotamba Ulaya.

Baadhi ya majina makubwa yanayompa jeuri Deschamps ni Paul Pogba, Antoine Griezmann, Kylian Mbappe na Ousmane Dembele.

Deschamps anataka kushika nafasi ya tatu ya kutwaa ubingwa akiwa kocha na mchezaji kama ilivyokuwa kwa Mario Zagallo na Franz Beckenbauer .

“Tunajkwenda vitani tukiwa tukitambua kuna mataifa mawili ya Ulaya Hispania na Ujerumani, pia lipo Taifa moja kutoka Korea Kusini (Brazil),” alisema Deschamps.

Ujerumani

Ujerumani ina timu yenye wachezaji wakongwe wenye uzoefu wa kutosha na michuano ya kimataifa.

Lakini, uwepo wa kundi la wachezaji chipukizi kina Timo Werner, Leon Goretzka na Joshua Kimmich, umeongeza matumaini kwa timu hiyo kufanya vyema.

“Ujerumani tutakuwa tunawindwa, kama tunataka kuwa mabingwa tena ni lazima tuongeze kasi.