In Summary
  • Akizungumza na Bambika 101, Rais wa Mtandao wa Wasanii wa Injili Tanzania (Tagoane), DK Godwin Maimu alisema pamoja na mambo mengine wasanii hao watapata nafasi ya kushinda kwa siku nzima na watoto yatima.

Tamasha kubwa la mwisho wa mwaka la ‘Tanzania Tukuza Utalii Festival’ litakalofanyika kwa siku sita mkoani Arusha linatarajia kuwaunganisha waimbaji lukuki wa muziki wa injili, akiwamo Angel Bernard, Joel Lwaga, Masanja Mkandamizaji na Shadrack Robert.

Akizungumza na Bambika 101, Rais wa Mtandao wa Wasanii wa Injili Tanzania (Tagoane), DK Godwin Maimu alisema pamoja na mambo mengine wasanii hao watapata nafasi ya kushinda kwa siku nzima na watoto yatima.

Aliwataja wanamuziki wengine kuwa ni Walter Chilambo, Paul Clement, Jordan Band, Gospel Comedy ikiongozwa Bambo pamoja na wengine wengi kutoka katika mikoa mbalimbali nchini.

Dk Maimu alisema wameandaa tamasha hilo litakalofanyika mkoani Arusha ili kuwaunganisha wanamuziki ambao mara nyingi wamekuwa wakikosa nafasi ya kuzungumzia masuala yanayowahusu. “Tumeandaa siku ya tamasha, kushinda na watoto yatima, kutembelea hifadhi zetu za kitalii na hata kukaa na kuzungumza pamoja kuhusu masuala yetu ya muziki, utakuwa wakati mzuri zaidi kwa wasanii wetu wa muziki wa injili,” alisema.

Alisema licha ya kuwaunganisha alisema lengo hasa ni kuwakumbusha wanamuziki umuhimu wa kupendana, kujali makundi mengine pia kuenzi utalii kupitia

Dk Maimu aliongeza kuwa sio tu kwa wanamuziki wenye majina makubwa peke yao, kongamano hilo litawaunganisha wanamuziki wachanga walioingia kwenye fani hiyo, siku za karibuni.

Mwanamuziki, Shadrack Robert alisema suala la wanamuziki kukutana na kushirikiana kwenye masuala mbalimbali ya kijamii na hivyo kujenga umoja.