In Summary
  • Anapozuiwa kufanya kazi zake kwa uhuru, na hasa anapofuatiliwa katika kila jambo analofanya, au kunapokuwa hakuna ushauri (consultation) ya kutosha kuhusu kazi za kila siku.

Msongo unaotokana na muundo na mwelekeo wa ofisi.

Huu hutokea wakati mfanyakazi anapokuwa hana kabisa au kuwa na ushiriki mdogo katika maamuzi ya ofisi, na hasa yanayomhusu.

Anapozuiwa kufanya kazi zake kwa uhuru, na hasa anapofuatiliwa katika kila jambo analofanya, au kunapokuwa hakuna ushauri (consultation) ya kutosha kuhusu kazi za kila siku.

Kwa ujumla, mambo hayo yote yaliyotajwa hapo juu hupelekea mfanyakazi kuwa na wasiwasi kazini, kutojiamini na kushindwa kuvumilia magumu ya kazi.

Kwa pamoja huwa na dalili kama mapigo ya moyo kuongezeka, kuongezeka kwa kolestro mwilini, uvutaji wa sigara uliozidi, kuwa mpweke, ulevi wa “kupunguza” mawazo, kutofurahia kazi na kupungua kwa msisimko wa kazi.

Mfanyakazi kama huyu mara nyingi hupenda kuzungumzia hamu yake ya kuacha kazi na kujiunga na kampuni au ofisi nyingine.

Mfanyakazi mwajiriwa kuwa na maswali ambayo mara nyingi hukosa majibu na kupelekea msongo wa mawazo.

Mfano wa maswali hayo ni mara ngapi huwa mwajiriwa anajisikia hana, au hajui uzito na umuhimu wa majukumu yanayoandamana na kazi yake, wakati mwingine mwajiriwa hujifikiria kama asiye na vigezo vya kutosha kwa kazi aliyo nayo, au wakati mwingine hukosa taarifa anayoihitaji ili kazi yake ifanikiwe.

Pia ni kawaida mwajiriwa kuwa na wasiwasi kwa jinsi wafanyakazi wenzake wanavyomchukulia, mathalani, wanampenda au wanamchukia? Na pia humpa wakati mgumu mwajiriwa kufikiri kuhusu yale watu waliomzunguka wanayotegemea kutoka kwake.

Njia pekee ya kuzuia aina hii ya msongo wa mawazo ni kwa kupunguza uzito wa vyanzo vyake katika kazi.

Kwa wale ambao kazi zao ni nyingi kupita uwezo wao, wanapaswa au kugawa majukumu kwa wengine au kuwa na siku fulani za kupumzika na kuwa na familia zao.

Hilo husaidia akili ya mfanyakazi kupata muda wa kupumzika na hivyo kupunguza uwezekano wa kupata msongo wa mawazo.

Imebainika kuwa, waajiriwa wengi hasa vijana wenye umri kati ya miaka ishirini na thelathini na tisa wangependa kufanya kazi zinazotoa muda wa kutosha kwa wao kuwa na familia zao kuliko kazi ngumu au kazi zenye mshahara mkubwa inazowanyima muda wa kuwa na familia zao.

Maofisi mengine hutoa likizo fupifupi za mara kwa mara kwa wafanyakazi wake ili kuwapunguzia mawazo kuhusu watoto.

Maofisi mengine hata yameanzisha shule kwa ajili ya watoto wa wafanyakazi wake, lengo ikiwa ni kupunguza msongo wa mawazo kwa wafanyakazi.

Hii imesaidia kuimarisha utendaji kazi wa waajiriwa katika maofisi hayo na maofisi hayo kujihakikishia faida zaidi. Kwa sababu ni ukweli usiopingika kuwa, pamoja na magumu mengi ya maisha, watu wengi hupata tulizo la moyo pale wanapokuwa na familia zao, na hasa wanapoona familia zao zina amani na furaha.

Waajiriwa au wafanyakazi wengi hutoa ripoti ya msongo wa mawazo hasa malengo ya kazi wanazofanya kutoeleweka, wanapopewa majukumu yanayogongana kiutekelezaji, majukumu kidogo sana au mengi sana, wanapohusika kidogo sana kwenye maamuzi muhimu hasa yanayowagusa na kuwahusu na wakati wanapokuwa na wajibu wa kuwasaidia wafanyakazi wengine kupanda madaraja kikazi wakati wao wako palepale.

Msongo utokanao na matatizo yanayoandamana na nafasi ya kazi.

Mfanyakazi anapokuwa na uhakika kuwa nafasi yake ya kazi inathaminiwa, humpa unafuu wa kazi na pia humpunguzia msongo wa mawazo.

Matatizo kama kazi kuwa nyingi wakati muda ni finyu, mgongano wa majukumu na hasa mabosi wawili wanapotaka vitu tofauti kutoka kwa mfanyakazi mmoja. Pia, uwezo wa mfanyakazi unapokuwa mdogo kulingana na umuhimu wa kazi yenyewe na hasa matazamio ya ofisi yanapokuwa makubwa wakati mfanyakazi anajiona hana huo uwezo, msongo wa mawazo unaweza kumpata kirahisi.

Kingine ni mwajiriwa kutokuridhika na kazi aliyonayo. Hii husababishwa na mambo mengi yakiwamo mshahara kuwa mdogo ukilinganisha na kazi anayofanya mtu pamoja na huduma muhimu katika mazingira ya kazi. Mfano, kunapokuwa na kelele nyingi, mwanga mdogo, hewa kuwa kidogo au wanapofanya kazi wafanyakazi wengi katika eneo dogo. Lakini, la muhimu pengine kuliko yote ni jinsi ofisi linavyomjali huyu mfanyakazi. Hii ni kwa kazi anazozifanya, je zinathaminiwa? Huwa mfanyakazi anatiwa moyo sana katika kutekeleza majukumu yake kama anahisi yeye na kazi yake kuthaminiwa?