In Summary
  • Kylie ana ujauzito wa miezi mitano
  • Khloe ana ujauzito wa miezi mitatu
  • Ujauzito wa Kim uliobebwa na mwanamke mweingine una miezi mitano

Familia ya Kardashian haiishi kupamba vichwa vya habari. Wiki hii katika siku tatu dada wawili wa familia hiyo, Khloe na Kylie walitangaza kuwa na ujauzito wakipeana siku moja katikati kutofautisha matangazo hayo. Habari hizo zimepamba kurasa mbalimbali za habari duniani kutokana na sababu kuu tatu.

Sababu ya kwanza ni umri wa Kylie aliyekuwa wa kwanza kutangaza kuwa mjazito. Ndiye mtoto wa mwisho katika familia hiyo ambaye ametimiza miaka 20 hivi karibuni. Sababu ya pili ni Khloe kutajwa kuwa ‘mgumba’ kwani pamoja na kuwa na umri wa miaka 34 hajawahi kushika ujauzito na mara zote amedai kuwa anatafuta mtoto kwa udi na uvumba.

Sababu ya tatu iliyofanya habari hiyo iwe kubwa ni uhusiano wa ujauzito huo wa ndugu wawili na ule wa dada yao, Kim ambaye miezi kadhaa nyuma alitangaza kuwa kuna mwanamke amebeba ujazito wake (sarrogate mother).

Baada ya Kylie na mpenzi wake Travis Scott kutangaza kuwa wanatarajia mtoto, Mtanzania ulizizima kuwa huenda ndiye surrogate mother wa Kim. Kwamba  Kim na mumewe Kanye West wamepandikiza ujauzito katika tumbo la mdogo wake huyo.

Uwiano wa namba ndio unawafanya watu waamini inawezekana Kylie amembebea dada yake ujauzito. Kylie ana ujauzito wa miezi mitano na mwanamke aliyebeba ujauzito wa Kim vivyo hivyo. Pia, Kim anatarajia mtoto wa kike na Kylie vivyo hivyo.