In Summary

Daddy Yankee anaungana na Jennifer Lopez ambaye naye majuzi alitangaza kuchangia dola za Marekani 1 milioni.

Baada ya kimbunga Maria kukipigi kisiwa cha Puerto Rico, mastaa mbalimbali wamejitokeza kuchangia na jana mwanamuziki Daddy Yankee ametangaza kuwa atatoa kiasi cha dola za Marekani 1 milioni  kwa aajili ya kuchangia shughuli za uokoaji.

Daddy Yankee anaungana na Jennifer Lopez ambaye naye majuzi alitangaza kuchangia dola za Marekani 1 milioni ambazo ni wastani wa Sh2.4 bilioni.

Mbali na kiasi hicho Daddy Yankee ameahidi kutoa dola laki moja kwaajili ya Shirika la Red Cross ambalo linafanya kazi ya uokoaji.

Pi a amewaomba mashabiki kuendelea kutoa michango kwa kuwa wakazi wengi hawana huduma muhimu kutokana na miundo mbinu kuharibiwa vibaya.