In Summary

Mrembo na nyota wa muziki wa Injili, Angel Bernad amejifungua mtoto wa kike.

Mrembo na nyota wa muziki wa Injili, Angel Bernad anayetamba na wimbo wa ‘Sitetereki’ amejifungua mtoto wa kike katika hospitali ya Mount Meru, jijini Arusha.

Mumewe Godsave Sakafu aliposti kwenye kurasa zake za Istagram na facebook kuwa mkewe Angel na mtoto wao wapo salama.

“Mungu ametuongeza tena, ametubariki ‘Its a baby girl’, mke wangu na mtoto wapo salama ‘it’s a baby girl’,”aliandika Sakafu akimaanisha kwamba, ni mtoto wa kike.

Miongoni mwa kazi anazotamba nazo mwanamuziki huyo ni pamoja na ‘Nikumbushe’ na ‘Salama’ na hivi karibuni alitikisa dunia baada ya kufanya kolabo na mwanamuziki nyota nchini Kenya Mercy Masika.