In Summary

Nyota huyo yupo sanjari na Victoria Kimani, ambapo kwa siku nne sasa wanaendelea kurekodi kipindi hicho kinachotarajiwa kuonekana baadaye mwaka huu.

Dar es Salaam. Msimu wa tatu wa onyesho la Coke Studio unatarajiwa kuanza hivi karibuni, huku nyota wa muziki wa Bongo Fleva, Ali Kiba akiwa jijini Nairobi akirekodi vipindi hivyo.

Nyota huyo yupo sanjari na Victoria Kimani, ambapo kwa siku nne sasa wanaendelea kurekodi kipindi hicho kinachotarajiwa kuonekana baadaye mwaka huu.

Ali Kiba ni mmoja kati ya wasanii wengine wakubwa wa Bongo wanaotarajiwa kujumuika katika msimu huu wa Coke Studio. Kwa mujibu wa waandaaji onyesho la, msimu huu litawakusanya pamoja wasanii kutoka Tanzania, Kenya, Uganda, Msumbiji na Nigeria.

Nyota wengi kutoka Bongo wameonekana jijini Nairobi hivi majuzi akiwamo Ommy Dimpoz aliyefanya ‘collabo’ na Avril katika wimbo wa “Hello Baby”, ambaye pia ana wimbo mpya uitwao “Wanjera”. Dimpoz aliyekuwa ameambatana na Idris Sultan mshindi wa Big Brother Africa 2014, walizuru maeneo mbalimbali ya jiji hilo.

Ommy Dimpoz amewaweka katika hali tete mashabiki wake Afrika Mashariki kwa wanaodai kwamba huenda ataonekana pamoja jukwaani na Avril msimu huu.

Hata hivyo, waandaaji wa Coce Studio wamedai kuwa Wakenya wengi wanatarajia wasanii nyota wa Bongo kushiriki msimu huu ili kujumuika nao pamoja.

Waliovuma katika msimu uliopita ni pamoja na Vanessa Mdee aliyeshiriki wimbo wake “Closer” akiwa na Burna Boy wa Nigeria na Diamond aliyeshirikiana na Yemi Alade kufanya remix ya “Johnny