In Summary

Kauli hiyo ya NHC imekuja siku chache baada ya kumtimua Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe katika jengo la Billcanas na kuahidi kufanya hivyo kwa wadaiwa sugu.

Dar es Salaam. Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) limesema baadhi ya wadaiwa sugu tayari wamelipa madeni yao na wengine wameonyesha nia  hivyo hawatatimuliwa.

Kauli hiyo ya NHC imekuja siku chache baada ya kumtimua Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe katika jengo la Billcanas na kuahidi kufanya hivyo kwa wadaiwa sugu.

Mkurugenzi wa Kitengo cha Mawasiliano wa NHC, Susan Omary amesema baadhi ya wadaiwa ambao hakuwataja majina wameshalipa, wengine wanaendelea kulipa na baadhi wametoa ahadi.

Kwa mujibu wa NHC, baadhi ya wadaiwa ni Wizara ya Ujenzi (Sh2 bilioni); Wizara ya Habari (Sh1 bilioni); Wizara ya Mambo ya Nje (Sh613 milioni); Tume ya Utumishi (Sh109 milioni) na Benki ya Azania (Sh161 milioni).