In Summary
  • Uzinduzi wa simu hiyo nchini unatarajiwa kufanyika Novemba 11 na utakwenda sambamba na kukabidhi simu kwa wateja walioweka ‘oda’ katika duka la Mlimani City jijini Dar es Salaam.

Dar es Salaam. Baada ya kampuni ya utengenezaji wa simu ya Tecno kuzindua simu mpya aina ya Phantom 8 nchini Dubai, baadhi ya wateja wameanza kutoa ‘oda’ zao kabla ya uzinduzi hapa nchini.

Uzinduzi wa simu hiyo nchini unatarajiwa kufanyika Novemba 11 na utakwenda sambamba na kukabidhi simu kwa wateja walioweka ‘oda’ katika duka la Mlimani City jijini Dar es Salaam. Ofisa uhusiano wa Tecno, Erlick Mkomoya alisema wateja wengi wamevutiwa na uwezo wa simu hiyo iliyo tofauti na matoleo yaliyotangulia. “Baada ya kuzinduliwa Dubai, tulilazimika kuanzisha zoezi la uwekaji oda za simu hizo Oktoba 26 katika duka letu baada ya watu kuonekana kuwa na shauku ya kuzitumia pindi tu zitakapoingia nchini,” alisema Mkomoya.

Mfanyabiashara katika soko la Kariakoo, Hamidu Rahim alisema utaratibu wa uwekaji ‘oda’ unawasaidia watu wenye kipato kidogo kumudu gharama.