In Summary
  • Kiwanda hicho kitatosheleza mahitaji ya hospitali zote nchini tofauti na sasa   zinaangizwa nje ya nchi.

Bariadi. Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) umeonyesha utayari wa  kujenga kiwanda cha kutengeneza bandeji na dripu mkoani Simiyu.

Kiwanda hicho kitatosheleza mahitaji ya hospitali zote nchini tofauti na sasa   zinaangizwa nje ya nchi.

Akizungumza kwenye kikao cha Kamati ya Ushauri ya Mkoa (RCC) jana, Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Anthony Mtaka amesema ni aibu kwa Tanzania kuendelea kuagiza bidhaa nje ya nchi ambazo inawezekana kutengenezwa nchini.