In Summary
  • Alitoa kauli hiyo jana alipohojiwa kuhusu kufutiwa leseni ya biashara na kufungiwa kwa benki tano na tatu kuwekwa chini ya uangalizi.

Arusha. Aliyewahi kuwa Gavana wa Benki Kuu (BoT), Edwin Mtei ametahadharisha juu ya uwapo wa benki nyingi nchini akisema wingi wa taasisi hizo unaongeza hatari katika sekta ya fedha.

Alitoa kauli hiyo jana alipohojiwa kuhusu kufutiwa leseni ya biashara na kufungiwa kwa benki tano na tatu kuwekwa chini ya uangalizi.

“Kuzifuta baadhi ya taasisi ni mambo yanayotokea kwenye nchi zenye benki nyingi,” alisema.